CHANGAMOTO


Maji salama ya kunywa ni msingi kwa afya bora katika maisha. Magonjwa mengi yanasababishwa na machi machafu.
 
Kila siku, watu 4000 wanakufa kutokana na madhara ya kunywa maji machafu ; haki ya kila binadamu kupata maji salama bado haijawa uhakika kwa sehemu nyingi hapa duniani.

Ukiachana na magonjwa makuu, kuna madhara mengine kama vile kukosa kwenda kazini au shule. Zaidi pia, matibabu ni gharama sana na yanaweza kusababisha kufirisika kifedha.  

SULUHISHO


Chujio la Maji imetengenezwa kutokana na rasilimali za ndani na kufanya kupata maji safi na salama ya kunywa. Chujio la maji linatengenezwa na kuuzwa katika maduka ya chujio za maji katika bei ya kawaida.

Mradi wetu wa majaribio upo Kigoma, Tanzania. Sehemu ya uzalishaji unasimamiwa na kutekelezwa kwa kuhusisha mashine zote muhimu na miundombinu mizuri. Mtandao wa mashirika yasiyo ya kifaida mbalimbali (hasahasa MIBOS) tunashirikiana nao kwa karibu kwenye mradi huu.

Ukichukulia miundombinu ya kimkoa, tumegundua maono yetu ya kuwawezesha watu kushiriki katika ujasiliamali, utawezesha wao kupata maji salama ya kunwa.

NUNUA CHUJIO LAKO LA MAJI HAPA

FAIDA 3 KUU


MAJI SAFI

Chujio la maji tunalotumia limetengenezwa na mashine. Pia limetengenezwa na rasilimali za ndani kama vile udongo na maganda ya mchele. Ufanisi wake wa asilimia 99.9 umepimwa na kuthibitishwa na tafiti mbalimbali za machujo ya maji mfano mzuri ni ule uliofanywa na MIT. Usimamizi wa ubora wake kwa muda mrefu unawezwa kuhakikishwa na wajasiliamali wa maji kama wakifundishwa katika uwanja huu vizuri.

AJIRA

Wajasiliamali wanafanya kazi katika kituo cha uzalishaji kutengeneza na kuuza chujio za maji. Pia wanahusika katika usimamizi wa ubora kama ilivyo ainishwa, ambapo inahusisha matengenezo na mafunzo ya ufahamu kuhusu chujio za maji. Kwa muda mrefu, dhana ya mfunzaji wa mafunzwa imepangwa. Kwa njia hii, uzoefu na pia maarifa vinawezwa shirikishwa kuleta ukuaji wa uchumi na ajira.

ELIMU

Sehemu kuu katika mradi wetu ni kufundisha na kuhamasisha ufahamu juu ya maji safi na salama. Kufanikisha hili kwa ufanisi tunafikia mashule ndani ya mkoa na kufanya miradi kuhusiana na maji ili kufikia uelewa erevu. Maarifa yatokanayo yatashirikisha familia na marafiki. Pia tunataka kutumia njia za mawasiliano kufikia watu kupitia makanisa au vituo vya afya.


 Maono yetu ni kuwezesha jamii kupata maji ya kunywa safi na salama kwa nguvu ya ujasiliamali.

Pata kutujua sisi


Nunua chujio lako la maji!

Sisi ni nani


TIMU YETU

Sisi ni timu a wanafunzi kutoka Ujerumani jiji la Munich, wenye chimbuko la fani mbalilmbali. Dhumuni letu ni kufanya dunia sehemu nzuri kwa kuwawezesha watu wasio na bahati kupitia njia ujasiliamali endelevu, mwishowe kuwawezesha kuishi maisha bora!

Washiriki wetu wakuu